Jumapili, 4 Februari 2018

HABARI ZA MASTAA>>ZARI KAAMUA KUUFANYA HIVI HADI KWA NDUGU WA DIAMOND PLATINUMS.

Mahusiano ya staa wa Bongo fleva Diamond Platnums yana zidi kugonga vichwa hasa kwa mashabiki zake kila kukicha,ni baada ya mfurulizo wa matukio  ya Diamond platnums ,yanayo daiwa kumkela Mzazi mwenzake Zari hususani ukaribu wake na Wema Sepetu hivi karibuni na kuamua kumunfollow Diamond kwenye  mtandao wa kijamii wa instagram pamoja na mama yake Diamond na ndugu wengine wa Diamond.
Wema Sepetu alisha wahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na staa huyo. 

MICHEZO>>REAL MADRID WATOKA SARE NA LEVANTE 2-2.

Club ya Real Madrid ya Hispania usiku wa Jana  February 3 2018 imedhihirisha kuwa sasa ni rasmi haipo katika mbio za kuwania Ubingwa wa LaLiga hivyo inapambana kumaliza katika nafasi mbili za juu hiyo ya sare ya goli 2-2 dhidi ya Levante .

Real Madrid ambao walikuwa ugenini dhidi ya wenyeji wao Levante katika uwanja wa Ciutat de Valencia wao ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 11 kupitia kwa Ramos ,Levante  wakasawazisha goli hilo dakika ya 42 kupitia kwa Boateng. 

 Real madrid walikuwa wanamiliki mpira kwa kiasi kikubwa, baada ya kufanikiwa kupata goli la pili dakika ya 81 Isco akifunga goli hilo , Real madrid furaha yao iliharibika dakika moja kabla ya mchezo kuisha pale Pazzin alipo sawazisha goli lapili timu yake ya Levante na kupelekea kutoka sare katika mchezo huo.

HABARI ZA MAGAZETINI>>MAGAZETI YA LEO FEBRUARY 4,2018 JUMAPILI.




























Jumamosi, 3 Februari 2018

BURUDANI>>CASSPER NYOVEST AMEWAAMBIA MASHABIKI ZAKE WAKAE TAYARI KWA KITU KIPYA.

Msanii kutoka nchini Afrika kusini Cassper Nyovest ameweka picha kwenye ukurasa wa instagram akiwa pamoja na msanii Swizz Beats kutoka nchini Marekani na kuwajulisha mashabiki kuwa kuna wimbo mpya unakuja.

" Unapojaribu kupanga wimbo na swizz Beatz lakini bado hujui.Haahaaa hi picha inachekesha"maneno ya Cassper Nyovest.

HABARI>>RAIS DR.JOHN MAGUFULI AMEWATUNUKU KAMISHENI MAAFISA WAPYA WA JWTZ KUWA LUTENI USU.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli leo February 3 ,2018 amewatunuku kamisheni maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania  JWTZ 197 kuwa Luteni Usu ,kati ya hao wanawake wakuwa ni 28 katika shughuli iliyofanyika kwenye viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Katika Sherehe hizo  viongozi mbalimbali wa serikali,wameudhia  akiwemo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Waziri mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Ulinzi na Usalama, Dr. Hussein Mwinyi na  Mkuu wa Majeshi ya Tanzania, General Venance Mabeyo, wakuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama wastaafu  na viongozi wa majeshi ya nchi jirani ambao baadhi ya wanajeshi wao wametunukiwa leo kutoka Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi na nchi nyingine rafiki.

UTAFITI>>SAMAKI MWENYE UWEZO WA KUONGEA KAMA BINADAMU ,UFARANSA.


             
Wataalamu nchini Ufaransa wameshangazwa na Nyangumi mwenye uwezo wa kutamka baadhi ya maneno ya binadamu , jambo ambalo ni nadra kutokea
Inaelezwa kuwa Nyangumi huyo ambaye anaweza kuwa amejifunza na kuweza kutamka maneno ya ‘hello’, ‘Amy’, ‘one’, ‘two’ na ‘three’. Wataalamu wanaeleza  Nyangumi ni miongoni mwa wanyama wachache tofauti na binadamu wanaoweza kujifunza kutoa sauti za matamshi kwa kuyasikia tu.
Nyangumi huyu alifundishwa kuongea maneno ya binadamu kupitia shimo lake la kupumua na anaweza kusikilizwa kwenye sauti yake iliyorekodiwa akirudia maneno kwa sauti ya kelele, ya kunong’oneza ama sauti laini.


Ijumaa, 2 Februari 2018

MICHEZO>>BAADA YA MKATABA WA OZIL NA ALEXIS SANCHEZ ,HII NDIYO ORODHA YA WACHEZAJI WANAOLIPWA ZAIDI.

Mesut Ozil anaonekana kupata kile akitakacho,kwa muda sasa kiungo huyo wa Kijerumani amekuwa akidai nyongeza ya mshahara na sasa atakuwa akipewa mara mbili ya mshahara wake wa mwanzo.
Ozil alikuwa akilipwa £150,000 kwa wiki lakini mkataba wake mpya na Arsenal utamfanya kuanza kupokea £300,000 kwa wiki pesa ambayo inamfanya kiungo huyo kuwa kati ya wachezaji 10 wanaolipwa zaidi EPL.
Ozil yuko nafasi ya pili ya wachezaji wanaolipwa zaidi EPL na ni nyuma ya mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Alexis Sanchez ambaye kwa sasa baada ya kujiunga na Manchester United anapokea £350,000 kwa wiki na ndio namba moja EPL.
Katika tatu bora ya wachezaji wanaolipwa zaidi EPL inaonekana Manchester United wana wachezaji wawili kwani ukiacha Alexis aliyeko nafasi ya kwanza yuko Paul Pogba katika nafasi ya 3 na anapokea £290,000 kwa wiki.
Kelvin De Bruyne ndiye mchezaji anayelipwa zaidi Man City na EPL yuko nafasi ya nne akiwa anapokea £280,000 kwa wiki akifuatiwa na Romelu Lukaku wa Manchester United anayepokea £250,000 kwa wiki.
Sergio Kun Aguero yuko nafasi ya sita akipokea kiasi cha £220,000 kwa wiki akifuatiwa na Yaya Toure ambaye pamoja na kuendelea kukaa benchi Manchester City lakini anapokea kiasi cha £220,000 kila wiki.
Zlatan Ibrahimovich naye anapokea mshahara sawa na Kun Aguero pamoja na Yaya Toure kiasi cha £220,000 akifuatiwa na David De Gea anayepokea £200,000 kwa wiki sawa na Eden Hazard wa Chelsea .