Wataalamu nchini Ufaransa wameshangazwa na Nyangumi mwenye uwezo wa kutamka baadhi ya maneno ya binadamu , jambo ambalo ni nadra kutokea
Inaelezwa kuwa Nyangumi huyo ambaye anaweza kuwa amejifunza na kuweza kutamka maneno ya ‘hello’, ‘Amy’, ‘one’, ‘two’ na ‘three’. Wataalamu wanaeleza Nyangumi ni miongoni mwa wanyama wachache tofauti na binadamu wanaoweza kujifunza kutoa sauti za matamshi kwa kuyasikia tu.
Nyangumi huyu alifundishwa kuongea maneno ya binadamu kupitia shimo lake la kupumua na anaweza kusikilizwa kwenye sauti yake iliyorekodiwa akirudia maneno kwa sauti ya kelele, ya kunong’oneza ama sauti laini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni