Jumamosi, 3 Februari 2018

HABARI>>RAIS DR.JOHN MAGUFULI AMEWATUNUKU KAMISHENI MAAFISA WAPYA WA JWTZ KUWA LUTENI USU.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli leo February 3 ,2018 amewatunuku kamisheni maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania  JWTZ 197 kuwa Luteni Usu ,kati ya hao wanawake wakuwa ni 28 katika shughuli iliyofanyika kwenye viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Katika Sherehe hizo  viongozi mbalimbali wa serikali,wameudhia  akiwemo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Waziri mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Ulinzi na Usalama, Dr. Hussein Mwinyi na  Mkuu wa Majeshi ya Tanzania, General Venance Mabeyo, wakuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama wastaafu  na viongozi wa majeshi ya nchi jirani ambao baadhi ya wanajeshi wao wametunukiwa leo kutoka Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi na nchi nyingine rafiki.

Hakuna maoni: