Ijumaa, 2 Februari 2018

MICHEZO>>BAADA YA MKATABA WA OZIL NA ALEXIS SANCHEZ ,HII NDIYO ORODHA YA WACHEZAJI WANAOLIPWA ZAIDI.

Mesut Ozil anaonekana kupata kile akitakacho,kwa muda sasa kiungo huyo wa Kijerumani amekuwa akidai nyongeza ya mshahara na sasa atakuwa akipewa mara mbili ya mshahara wake wa mwanzo.
Ozil alikuwa akilipwa £150,000 kwa wiki lakini mkataba wake mpya na Arsenal utamfanya kuanza kupokea £300,000 kwa wiki pesa ambayo inamfanya kiungo huyo kuwa kati ya wachezaji 10 wanaolipwa zaidi EPL.
Ozil yuko nafasi ya pili ya wachezaji wanaolipwa zaidi EPL na ni nyuma ya mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Alexis Sanchez ambaye kwa sasa baada ya kujiunga na Manchester United anapokea £350,000 kwa wiki na ndio namba moja EPL.
Katika tatu bora ya wachezaji wanaolipwa zaidi EPL inaonekana Manchester United wana wachezaji wawili kwani ukiacha Alexis aliyeko nafasi ya kwanza yuko Paul Pogba katika nafasi ya 3 na anapokea £290,000 kwa wiki.
Kelvin De Bruyne ndiye mchezaji anayelipwa zaidi Man City na EPL yuko nafasi ya nne akiwa anapokea £280,000 kwa wiki akifuatiwa na Romelu Lukaku wa Manchester United anayepokea £250,000 kwa wiki.
Sergio Kun Aguero yuko nafasi ya sita akipokea kiasi cha £220,000 kwa wiki akifuatiwa na Yaya Toure ambaye pamoja na kuendelea kukaa benchi Manchester City lakini anapokea kiasi cha £220,000 kila wiki.
Zlatan Ibrahimovich naye anapokea mshahara sawa na Kun Aguero pamoja na Yaya Toure kiasi cha £220,000 akifuatiwa na David De Gea anayepokea £200,000 kwa wiki sawa na Eden Hazard wa Chelsea .

Hakuna maoni: