Club ya Real Madrid ya Hispania usiku wa Jana February 3 2018 imedhihirisha kuwa sasa ni rasmi haipo katika mbio za kuwania Ubingwa wa LaLiga hivyo inapambana kumaliza katika nafasi mbili za juu hiyo ya sare ya goli 2-2 dhidi ya Levante .
Real Madrid ambao walikuwa ugenini dhidi ya wenyeji wao Levante katika uwanja wa Ciutat de Valencia wao ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 11 kupitia kwa Ramos ,Levante wakasawazisha goli hilo dakika ya 42 kupitia kwa Boateng.
Real madrid walikuwa wanamiliki mpira kwa kiasi kikubwa, baada ya kufanikiwa kupata goli la pili dakika ya 81 Isco akifunga goli hilo , Real madrid furaha yao iliharibika dakika moja kabla ya mchezo kuisha pale Pazzin alipo sawazisha goli lapili timu yake ya Levante na kupelekea kutoka sare katika mchezo huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni