Ijumaa, 2 Februari 2018

HABARI >>MWANASIASA MKONGWE KINGUNGE NGOMBALE MWIRU AMEFARIKI DUNIA LEO ALFAJIRI.

Asubuhi hii ya leo ya February 2, 2018  Mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amefariki dunia alfajiri ya leo.
Mzee Kingunge alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam takriban mwezi mmoja uliopita.

HABARI ZA MASTAA>>KINACHO ENDELEA KWENYE MSIBA WA MSANII RADIO ,UGANDA.


Siku ya Jana february 1,2018 zilisambaa  taarifa za kifo cha mwanamziki Radio kutoka nchini uganda aliye kuwa kwenye kundi la  Good lyfe ,ikiwa ni baada ya wiki mbili kulazwa ICU baada ya kupigwa na watu wasiojulikana katika moja ya kumbi za starehe nchini humo.




HABARI MAGAZETINI>>MAGAZETI YA LEO FEBRUARY 2 ,2018 IJUMAA.
































Alhamisi, 1 Februari 2018

BURUDANI>>DRAKE AMEVUNJA REKODI YA JAY-Z.

Drake anaendelea kuvunja rekodi, This Time kupitia nyimbo zake mbili “God’s Plan” na “Diplomatic Immunity” zimefanikiwa kuingia katika Top Ten ya chati za Billboard Hot 100 na kuvunja rekodi ya JAY-Z ya msanii wa Rap mwenye Top Ten nyingi zaidi katika chati za Billboard Hot 100.
Wimbo  God’s Plan unashikilia nafasi ya kwanza na “Diplomatic Immunity” nafasi ya saba, nakufanya Drake awe msanii aliyewahi kuwa na nyimbo 22 zilizoingia kwenye Top Ten ya Billboard Hot 100.
Pia rekodi hii imemfanya Drake kuwa msanii wa kwanza kuweka zaidi ya nyimbo mbili MARA mbili Kwa wakati mmoja kwenye Top Ten ya chati za billboard hot 100.
JAY-Z alikuwa akisikilia rekodi hii kwa wasanii wa Rap akiwa na nyimbo 21, Lil Wayne (20) , Ludacris (18), Eminem (17), Diddy (15), Nicki Minaj (15), T-Pain (15) na Kanye West (15).
Kwa wasanii wote kwa jumla Drake yuko sawa na Taylor Swift kwenye nafasi ya 13, Madonna (38), The Beatles (34), Rihanna (31),na Michael Jackson (29) wanaongoza.

HABARI>>WAANDISHI WA WA HABARI WA KITUO CHA NTV KENYA WAMELAZIMIKA KULALA OFISININI.


   
Waandishi watatu wa habari wa kituo cha Televisheni  NTV, Linus Kaikai, Larry Madowo na Ken Mijungu usiku wa jana wamelazimika kulala kwenye ofisi za kituo hicho cha televisheni kwa kuhofia kukamatwa na polisi kufuatia suala la kuapishwa  kwa Kiongozi Mkuu wa Upinzani NASA Raila Odinga.
Inaelezwa kuwa askari wasio na sare walikuwa wakizunguka nje ya jengo la kituo hicho kwa lengo la kuwakamata waandishi hao watatu kwa sababu ambazo bado hazikuwa .

MUCHEZO>>SAMUEL ETO´O AME VUNJA MKATABA NA TIMU YA ANTONLYASPOR NA KUJIUNGA NA TIMU HII.

Mchezaji wa kimataifa wa CameroonSamuel Eto´o ametangazwa kuvunja mkataba na Antonlyaspor ya Uturuki  na kuamua  kujiunga na club ya Konyaspor  ya Uturuki .
Samuel Eto´o alijiunga na Antalyaspor mwaka 2015 akiwa ameitumikia timu hiyo miaka miwili na mwaka huu 2018 ameamua kujiunga na Konyaspor baada ya kuvunja mkataba na timu hiyo kwa makubaliano ya pande zote mbili . 
Pia Eto´o alisha wahi kuchezea Fc Barcelona 2004 -2009 na kufanikiwa kushinda champions league mara tatu ,Pia alishawahi chezea vilabu kama Inter Milan,Anzhi Makhachkala ya Urusi,Chelsea ,Evarton na Sampdoria ya Italia kabla ya kwenda Uturuki. 

JPM AMESEMA YUPO TAYARI KUTEUA MAJAJI WENGINE ILI KUPUNGUZA UPUNGUFU WA MAJAJI.

Rais Dr.John Magufuli leo February 1, 2018 katika Maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Mahakama amesema yupo tayari kufanya uteuzi wa majaji wengine ili kukabiliana na changamoto ya upungufu mkubwa wa majaji ambayo inasababisha mrundikano wa mashauri katika Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani.
Pia  Rais Magufuli ametoa wito kwa Mahakama kuendelea kurekebisha dosari ambazo zimekuwa zikiuchafua mhimili huo wa Dola ikiwemo Majaji na Mahakimu kujihusisha na vitendo vya upokeaji wa rushwa na ucheleweshaji wa kesi ambavyo vinasababisha hasara kubwa kwa taifa.
Aidha amempongeza Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Juma kwa hatua ya kuwafukuza kazi watumishi 112 wa Mahakama wakiwemo Mahakimu 17 waliojihusisha na vitendo vya ukiukwaji wa maadili
Rais Magufuli ameeleza kushangazwa na vyombo vingine ambavyo hushirikiana na Mahakama kama vile Jeshi la Polisi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa "TAKUKURU" Magereza na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka DPP kwa kutowawajibisha watumishi wake wanaokiuka maadili.