Drake anaendelea kuvunja rekodi, This Time kupitia nyimbo zake mbili “God’s Plan” na “Diplomatic Immunity” zimefanikiwa kuingia katika Top Ten ya chati za Billboard Hot 100 na kuvunja rekodi ya JAY-Z ya msanii wa Rap mwenye Top Ten nyingi zaidi katika chati za Billboard Hot 100.
Wimbo God’s Plan unashikilia nafasi ya kwanza na “Diplomatic Immunity” nafasi ya saba, nakufanya Drake awe msanii aliyewahi kuwa na nyimbo 22 zilizoingia kwenye Top Ten ya Billboard Hot 100.
Pia rekodi hii imemfanya Drake kuwa msanii wa kwanza kuweka zaidi ya nyimbo mbili MARA mbili Kwa wakati mmoja kwenye Top Ten ya chati za billboard hot 100.
JAY-Z alikuwa akisikilia rekodi hii kwa wasanii wa Rap akiwa na nyimbo 21, Lil Wayne (20) , Ludacris (18), Eminem (17), Diddy (15), Nicki Minaj (15), T-Pain (15) na Kanye West (15).
Kwa wasanii wote kwa jumla Drake yuko sawa na Taylor Swift kwenye nafasi ya 13, Madonna (38), The Beatles (34), Rihanna (31),na Michael Jackson (29) wanaongoza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni