Alhamisi, 1 Februari 2018

JPM AMESEMA YUPO TAYARI KUTEUA MAJAJI WENGINE ILI KUPUNGUZA UPUNGUFU WA MAJAJI.

Rais Dr.John Magufuli leo February 1, 2018 katika Maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Mahakama amesema yupo tayari kufanya uteuzi wa majaji wengine ili kukabiliana na changamoto ya upungufu mkubwa wa majaji ambayo inasababisha mrundikano wa mashauri katika Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani.
Pia  Rais Magufuli ametoa wito kwa Mahakama kuendelea kurekebisha dosari ambazo zimekuwa zikiuchafua mhimili huo wa Dola ikiwemo Majaji na Mahakimu kujihusisha na vitendo vya upokeaji wa rushwa na ucheleweshaji wa kesi ambavyo vinasababisha hasara kubwa kwa taifa.
Aidha amempongeza Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Juma kwa hatua ya kuwafukuza kazi watumishi 112 wa Mahakama wakiwemo Mahakimu 17 waliojihusisha na vitendo vya ukiukwaji wa maadili
Rais Magufuli ameeleza kushangazwa na vyombo vingine ambavyo hushirikiana na Mahakama kama vile Jeshi la Polisi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa "TAKUKURU" Magereza na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka DPP kwa kutowawajibisha watumishi wake wanaokiuka maadili.

Hakuna maoni: