Jumamosi, 6 Januari 2018

MICHEZO:BABA MZAZI WA LIONEL MESSI AZUNGUMZA KUHUSU MESSI KUONDOKA BARCELONA

Baba mzazi wa Lionel Messi, Jorge Messi amezungumzia taarifa zinazosamba kuwa endapo jimbo la Catalonia litajitenga kutoka Hispania Messi ataachana na klabu hiyo kuwa ni taarifa za uongo.

Jorge ameyasema hayo kwenye mahojiano na kituo cha Radio Red  Argentina na kufafanua kuwa hakuna kipengele kinachotaka Messi aondoke Barcelona endapo Catalonia itajitenga na Hispania.
Taarifa hizo si za kweli ,mkataba mpya wa Messi hauna kipengele hicho, ila kuna maelewano yanayotaka pande zote mbili kuzingatia, Barcelona ni timu kubwa na inawachezaji wakubwa kwa hiyo inatakiwa kucheza ligi kubwa haijalishi ni ligi gani ila iwe moja ya ligi kubwa.

Messi alisaini mkataba mpya mwaka jana mwezi november wa kuendelea kubaki Camp Nou mpaka mwaka 2021.


share habari na marafiki zako kupitia# Rayv94.Blogspot.com.
Weka comments hapa.

Hakuna maoni: