Jumamosi, 6 Januari 2018

BURUDANI:UJIO WA FILAMU YA BRIGHT TOLEO LA PILI.



Baada ya kukosolewa filamu ya BRIGHT na mashabiki na kampuni kubwa ya filamu na show za Tv ya Netflix imethibitisha ujio wa toleo la pili la filamu ya BRIGHT iliyo chezwa na Will Smith pamoja na Joel Edgerton.
Rapa Chance The Rapper ni miongoni mwa watu waliokosoa filamu Bright  kwa kusema Hapendi kuona filamu kama hizi zinaongelea ubaguzi wa rangi kwa kutumia viumbe vingine badala ya watu halisi.
Netflix wamesema walikuwa wanasubiri kuona mafanikio ya Bright Part 1 kabla ya kutangaza ujio wa Part 2, sasa wamethibitisha baada ya filamu hii kutazamwa kwa kulipia na watu zaidi ya milioni 11 kwenye tv tu katika nchi 190, bila kuhesabu waliotazama kwenye computer na simu.Bright Part 1 ambayo imegharimu kiasi cha dola milioni 90
Share habari na marafiki zako kupitia #Rayv94.Blogspot.com.
Acha maoni yako hapa.

Hakuna maoni: