Staa mkubwa wa Rap na HipHop duniani DMX amewekwa jela baada ya kufeli vibaya vipimo vya matumizi ya dawa za kulevya.
DMX amevunja masharti ya Probation yake baada ya kukutwa na dawa za kulevya kwenye damu na mkojo wake, ni dawa aina ya Opiates, Cocaine na Oxycodone.
Wakili wa Serikali Nicholas Biase ametumia kama ushahidi video ya DMX akihubiri neno la Mungu huku akiwa amelewa katika kiwanja cha ndege cha St. Louis.
Wakili wa DMX , Murray Richman amesema amesikitishwa na tabia za mteja wake na atahakikisha anachukua hatua sawa za kumsaidia.
November mwaka jana, DMX alikiri makosa 14 ya ukwepaji kodi na kukwepa kwenda jela kwa kifungo cha miaka 40 badala yake jaji alikubali rapa huyu atumikie miaka mitano jela kifungo ambacho kitaanza March 29, 2018
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni