Mama aliye kuwa akifanya kazi mahakama iliyosimamia kesi ya Meek Mill ‘Wanda Chavarria’ amefukuzwa kazi baada ya kuomba mchango wa ada ya mwanae kutoka kwa rapa huyo.
Wanda Chavarria aliandika barua fupi na kuipenyeza kwa Meek Mill kama njia ya kuomba mchango wa rapa huyo ili aweze kumaliza malipo ya mtoto wake ambaye yuko kwenye mwaka wa mwisho wa chuo.
Chavarria pia amethibitisha kuwa jaji wa kesi hio Judge Genece Brinkley hakujua kuhusu kitendo chake cha kuomba msaada mtuhumiwa aliyekuwa na kesi kwenye mahakama hio.
Kutokana na kuvunja masharti aliyowekewa akiwa uraiani na chini ya uangalizi wa polisi Meek Mill alihukumiwa tena kifungo cha miaka miwili mpaka minne.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni