Jumatano, 31 Januari 2018

MAAGAIZO YA ALIYO YATOA RAIS WA LIBERIA GEORGE WEAH KWA MARA YA KWANZA KATIKA HOTUBA YAKE.

Rais wa Liberia George Weah ameagiza kutolewa kwa kipengele kinachoonyesha ubaguzi kwenye katiba ya nchi hiyo, ambacho kinaruhusu upatikanaji wa uraia kwa watu weusi tu.
Ametoa agizo hilo katika hotuba yake ya kwanza kwa Waliberia tangu achaguliwe kuwa Rais. Weah amesema vikwazo na vipingamizi vyote hivi viliwekwa wakati ambao havikuwa vinahitajika tena.
"kipengele hicho ni cha kibaguzi na hakina maana yoyote" Rais George Weah.
Katiba ya Liberia  inamtambua mtu mweusi kwa jina la Negro jina la kibaguzi walilokuwa wakiitwa watu weusi wakati wa utumwa.
George Weah ameahidi pia kufuta sheria inayowazuia wenyeji kumiliki ardhi. Watu kutoka mataifa mbalimbali hasa raia 4,000 wa Lebanon wanaishi nchini Liberia kwa miaka kadhaa, lakini wamenyimwa uraia na haki ya kumiliki ardhi.

Hakuna maoni: