Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi katika Wizara ya Madini amemteua Doto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya mawasiliano ya Rais Ikulu, Doto Mashaka Biteko ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe na alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya muda iliyochunguza madini ya Tanzanite.
Kufuatia uteuzi huu alioufanya Rais JPM Wizara ya Madini itakuwa na Waziri na Manaibu waziri wawili.
Rais Magufuli amefanya uteuzi huu kwa lengo la kuongeza nguvu ktk wizara hiyo kutika na wingi wa majukumu katika Wizara ya Madini.
Doto Mashaka Biteko ataapishwa Jumatatu tarehe January 8, 2018 saa 3:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Share habari na marafiki zako kupitia#Rayv94.Blogspot.com.
Acha Comment yako hapa..
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni