Bado siku zisizozidi 5 ili dirisha dogo la usajili la mwezi Januari liweze kufungwa, tayari wapo ambao wameshafanya sajili kubwa na pia wapo wanaokaribia kufanya hivyo, na vile vile tetesi ni nyingi sana.
Habari kubwa sana katika dirisha la usajili wikiendi hii ni Arsenal ambao wanatajwa kuwa mbioni kukamilisha uhamisho wa Pierre Aubameyang toka Dortmund ambapo inasemekana kwamba tayari wamekubaliana ada ya uhamisho.
Mwenyekiti wa PSG Nasser El Khaifi amewakatisha tamaa Real Madrid wanaomtaka Neymar kwa kusema kwamba ana uhakika 2000% kwamba mchezaji huyo hawezi kuondoka PSG siku za usoni.
Inasemekana kwamba klabu ya Chelsea iko mbioni kumchukua kocha wa zamani wa klabu ya Barcelona Luis Enrique kama mrithi wa Antonio Conte ambaye siku zake za kukaa Chelsea zimeanza kuhesabika.
Inaonekana kama Manchester City wanataka kusajili mchezaji nyota ambaye yuko EPL, baada ya kushindwa kwa Sanchez sasa matajiri hao wanatajwa kuhamia kwa Hazard na wako tayari kutoa kiasi cha £150m.
Manchester United wanaonekana kutaka kuibomoa Borussia Dortmund ambapo wana mpango wa kuwanyakua nyota wao wawili Christian Pullisic na Julian Weigl kwa pamoja na mpango huo wanataka kuutimiza mwezi huu au dirisha lijalo la usajili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni