Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2017/2018 imeendelea leo januari 28,2018 kwa michezo miwili , Simba walikuwa nyumbani uwanja wa Taifa walikicheza na Majimaji FC kutoka Songea wakati Singida United walikuwa wenyeji wa Prisons katika uwanja wa Namfua.
Simba wamefanikiwa kujizolea point tatu baada ya kuifunga Majimaji FC magoli 4-0, mabao ya Simba yakifungwa na John Bocco aliyefinga magoli mawili dakika ya 16, 26 na Emmanuel Okwi naye akifunga magoli mawili dakika ya 52 na 68.
Ushindi huo umeifanya Simba kufikisha jumla ya point 35 na wakiwa na Magori 35, na kuendelea kuwa kileleni kwa point 35 ,wakifuatia na Azam FC wenye point 30 , na Singida United wameibuka na ushindi wa 1-0 vs Prisons wamesogea nafasi ya nne kwa kufikisha point 27.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni