share habari na marafiki zako# Rayv94.Blogspot.com.
Tayari Phellipe Coutinho yuko nchini Hispania na kilichobaki ni kuweka tu sahihi kwenye mkataba mpya na klabu ya Barcelona, huku Liverpool wenyewe wakineemeka kwa kiasi cha £142m walichopata.
Kiasi cha pesa walichonacho Liverpool ni kikubwa sana na wanaweza kufanya fujo kubwa kwenye soko la usajili, lakini nani wa kumsajili? Hapo ndipo ambapo Liverpool wanaweza kuwa katika mtego mkubwa.
Wakati Luis Suarez anaondoka kwenda Barcelona, Liverpool walikula £75m na ilitarajiwa pesa hiyo kuleta majina makubwa. Wakamnunua Divock Origi, Balotelli, Adam Lallana na Lazar Markovic lakini ni Lallana tu alifanikiwa.
Kuna mambo mawili yanaweza kuwatokea Liverpool katika kipindi hiki, moja wanaweza kutana na gharama kubwa ya wachezaji wanaowataka lakini pili wanaweza kununua wachezaji kwa bei kubwa na bado wakashindwa kutamba.
Wakati Cristiano Ronaldo anauzwa na United mwaka 2009, United walimtaka Benzema au Villa ili kuchukua nafasi ya Ronaldo lakini waliwakosa wote na baadae wakaangukia kwa Mame Diouf, Gabriel Oberten na Antonio Valencia.
Kuna faida kubwa kumtoa nyota mkubwa na kununua nyota mkubwa kwani achilia mbali kwamba mashabiki wanaridhika lakini inaijrnga “mentality” ya timu kushinda, wachezaji wanakuwa wanaelewa kweli timu inataka ushindi.
Coutinho ni jina kubwa na hadi wachezaji ndani ya Liverpool wanaelewa wamepoteza mchezaji mkubwa, unapomleta mchezani mdogo au wa kawaida wachezaji wanaelewa kwamba kumetoka mchezaji mkubwa na kumekuja mdogo.
Lemar anatajwa kwenda Liverpool na huu unaonekana unaweza kuwa usajili sahihi kwa Jurgen Klopp lakini pia ujio wa golikipa Jan Oblak kutoka Athletico Madrid unaweza kuwasaidia Liverpool kutuma message kwa wapinzani wao.
Tangu wakina Fernando Torres, Xabi Alonso, Raheem Sterling, Michael Owen waondoke Liverpool, klabu hiyo haijawahi kufanya usajili wa wachezaji wenye majina makubwa na pengine huu sasa ndio muda.
Source:Shaffii Dauda.
Naomba niachie maoni yako.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni